Uchambuzi wa Tawasifu ya Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa “Maisha Yangu, Dhamira Yangu: Rais wa Tanzania Akumbuka”

Mchambuzi: Prof. Rwekaza Mukandala

UTANGULIZI

Mtoto Benjamin William Mkapa, alifundishwa kupika chakula na mama mzazi Stephania akiwa mdogo. Alipokwenda shule hapo kijijini Lupaso, Ndanda na hatimaye St. Francis Pugu na Makerere, alifundishwa kupika, kufinyanga, kubuni na kuchambua mawazo na kuyaweka sawa kama msomi mbunifu na mwandishi. Kitabu hiki ni zao la mpishi wa mawazo mahiri aliyebobea.  Ni kitabu cha kurasa mia tatu na kumi na tisa, katika sura ya kumi na sita.   Kuna utangulizi ulioandikwa na Mheshimiwa Joaquim Chissano, Rais mstaafu wa Msumbiji, Pia kuna picha nyinge nzuri, na viambatisho viwili.  Mchapaji Mkuki na Nyota wamefanya kazi nzuri sana, sikubaini kosa hata moja.  

Wasilisho hili linamega simulizi hii katika sehemu kuu tatu. Kwanza tunapewa vionjo vitamu tukielezwa kuzaliwa kwake, kukua na kwenda shule. Hii ilikuwa matayarisho ya kufikia nia au azma yake ya maisha. Kisha tunaletewa mlo wenyewe (main course) uliosheheni kumbukumbu  na ngano za huyo kijana sasa mtu mzima akiwa kazini, mpaka akaukwaa urais wa Tanzania. Mwisho tunaelezwa kwa ufupi maisha yake baada ya kumaliza ngwe yake ya miaka kumi ya urais.

Soma zaidi: http://uongozi.or.tz/wp-content/uploads/2019/11/UCHAMBUZI-WA-MAISHA-YANGU-DHAMIRA-YANGU.pdf