Makamu wa Rais Philip Isdor Mpango kufungua kongamano la Jukwaa la Maendeleo Endelevu 2022

Mwanza: Mlezi wa Jukwaa la Maendeleo Endelevu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kufungua kongamano la mwaka huu la Jukwaa hilo, litakalojadili “Usimamizi madhubuti wa fukwe kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania”. 

Kongamano hilo, litakaloangalia masuala ya kisheria na kisera kwa ajili ya maboresho endelevu ya fukwe nchini, litafanyika kwa muda wa siku moja na nusu kuanzia tarehe 23 – 24 Novemba 2022. Litajumuisha mijadala ya kina na ziara katika mahali ambapo Mradi wa Tampere utatekelezwa. Mradi huo, ambao ni sehemu ya mpango kabambe (master plan) wa jiji la Mwanza (2015 – 2035), utahusisha ujenzi wa ofisi za serikali; maeneo ya bustani na viwanja vya michezo; hoteli, migahawa; majumba ya makumbusho na maonyesho; masoko; na ukumbi wa mikutano. 

Washiriki kwenye kongamano hili ni pamoja na Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora); Mhe. Mary Masanja, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii; wadau kutoka kwenye sekta za umma na binafsi, asasi za kiraia, taasisi za elimu ya juu; na washirika wa maendeleo. 

Jukwaa la Maendeleo Endelevu ni moja ya programu kuu za Taasisi ya UONGOZI katika masuala ya maendeleo endelevu. Lengo lake ni kukuza uelewa wa masuala ya uchumi wa kijani na mchango wake katika maendeleo nchini Tanzania. Linawakilisha zana ya kimaendeleo ya kujenga miunganisho ya kisekta, kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kutunza mifumo ya ikolojia na mazingira. Tangu kuzinduliwa (2010), makongamano saba yamefanyika. 

Ushiriki katika kongamano hili ni kwa mwaliko pekee. Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s